Musa mateja
WAKATI staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu akiweka wazi kuwa hawezi kupata ujauzito huku Judith Wambura ‘Jide’ naye akisumbuliwa na tatizo hilo, nyota wa muziki Rehema Chalamila, Ray C amefunguka na kusema kuwa hali ya kukosa mtoto ambayo ni sawa na ugumba, inamtesa, kwani katika umri wake wa miaka 33, hajabahatika kuwa naye,Risasi Jumamosi linakujuza.
Nyota wa muziki Rehema Chalamila, Ray C.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Ray C alisema kuwa pamoja na hamu yake ya muda mrefu ya kupata mtoto, lakini ameshindwa ingawa anaamini siku yoyote Mungu atamuwezesha jambo hilo.“Hao kina Jide, Wema mi naona kama ni cha mtoto. Katika uhusiano wangu wa kimapenzi tangu nivunje ungo, nimewahi kushika mimba mara moja tu, wakati huo nikiwa na Mwisho Mwampamba, lakini bahati mbaya ilitoka, tokea hapo sijapata tena,” alisema staa huyo ambaye yupo katika mapambano ya kuacha matumizi ya madawa ya kulevya.
Alisema katika umri wake huo anatamani sana kuwa na mtoto, kwani wasichana aliozaliwa nao wakati mmoja hivi sasa wanao watoto wawili hadi watatu, kitu ambacho kinamuumiza.Alipoulizwa kama matumizi ya dozi ya kuacha madawa ya kulevya inachangia tatizo lake hilo, alisema siyo kweli, kwani miongoni mwa ‘mateja’ wenzake anaokunywa nao dawa, wapo wajawazito na wengine wenye watoto.
Hata hivyo, alisema umri wake siyo mkubwa sana kukata tamaa ya kutozaa kwani wapo baadhi ya watu hupata ujauzito na kuzaa katika umri wa miaka 45 na kuendelea.“Sidhani kama umri ni sababu, nafikiri bado nina muda wa kuzaa na kumlea mwanangu nikijaaliwa kuwa naye, lakini pia huwa siishi kumshukuru Mungu kwa hivi nilivyo maana yawezekana kuna jambo ananiepusha nalo,” alisema.
“Kitu kingine kinachonifanya nisipate mtoto mapema ni pamoja na kutopata mwanaume aliyetulia ambaye ninaweza kuzaa naye, nadhani nikimpata mambo yanaweza kwenda vizuri.”Ray C anaingia katika orodha ya masupastaa ambao licha ya umri wao kuwa mkubwa, lakini bado hawajabahatika kupata watoto, baadhi yao wakiwa ni pamoja na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Baby Madaha na Jacqueline Wolper

Na SAST RECORDS
POMBE si chai! Msemo huu ulitimia hivi karibuni baada ya staa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ kuzidiwa na kilevi na kuanza kushindana kukata mauno na kusababisha azingirwe na wanaume waliovutiwa naye.
Staa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ akikata mauno.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumatano iliyopita katika sherehe ya bethidei ya mtoto wa msanii mwenzake, Halima Yahya ‘Davina’ iliyofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Lamada jijini Dar ambapo kulikuwa na vyakula na vinywaji vikali vya kila aina.
Nisha ambaye alikuwa amevalia kikaptula cha ‘jeans’ na kujistiri na mtandio, baada ya kukolea ulevi aliutupa mtandio na kuacha sehemu kubwa ya mwili wazi kisha  kukata mauno kushindana na mademu mcharuko waliokuwa ukumbini hapo kiasi cha kuwapagawisha wanaume wakware ambao walimvaa na kutaka kucheza naye.
Davina akiwa na mwanaye.
“Duh yaani Nisha leo ametia aibu, si kawaida yake nahisi mitungi imemzidi. Ameamua kujiachia kupitiliza, hebu mwangalie anavyokata mauno watoto wanamuangalia, aibu hii,” alisikika mualikwa mmoja akimwambia mwenzake.
Mauno mauno.
Hata hivyo, Davina alipoona baadhi ya waalikwa wanazidisha kusaula na kukatika, aliomba kipaza sauti na kuwataka wasifanye hivyo kwani sherehe ni ya mtoto.Sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa kibao akiwemo Jeniffer Kyaka ‘Odama’, Mayasa  Mrisho ‘Maya’, Mike Sangu, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wengine wengi ambao  baadhi yao walionekana wakiwa wamekolea kilevi

Sifael Paul
Hatari! Masistaduu wawili kunako gemu la Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper Massawe, wamejikuta wakipiga ulabu hadi kulewa chakari, kisa kikielezwa kwamba wana msongo wa mawazo, Risasi Jumamosi linafunguka.
Masistaduu wawili kunako gemu la Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper Massawe wakipiga mtungi usiku mnene.
ENEO LA TUKIO KINONDONI-MANYANYA
Tukio hilo lililoshuhudiwa na gazeti hili lilijiri hivi karibuni, usiku mnene kwenye pati ya kuzaliwa (birthday) ya meneja wa kampuni ya Wema ya Endless Fame almaarufu Petit Man iliyofanyika kwenye nyumba ya jamaa mmoja maeneo ya Kinondoni-Manyanya jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao.
Katika pati hiyo ambayo mbali na mastaa ilihudhuriwa na watoto wa mjini, watu waligonga msosi wa kufa mtu kisha vikafuata vinywaji.
Tofauti na ‘maraia’ wengine, Wema na Wolper walikuwa wakigonga vinywaji vikali hadi wakawa tilalila na kuanza kufanya vituko, jambo ambalo liliwashangaza wengi.Kadiri muda ulivyokuwa unasonga ndivyo mastaa hao walivyozidi kucharuka tofauti na walipofika kwani walionekana wapole na wastaarabu kupita maelezo.
Baada ya ulabu kuwakolea walianza kupigana picha kwa simu kisha kukata mauno kabla ya Wolper kuzimika kufuatia kuzidiwa na ‘kinywaji’.Kwa upande wake Wema alimpiga vibao mwanaume shoga aliyetajwa kwa jina moja la Danny baada ya kutibuana kabla ya watu kuwaamulia.Ulipofika muda wa kuondoka mahali hapo, ilidaiwa kwamba Wolper ilibidi abebwe ili kupelekwa kwenye gari kwani alikuwa hajiwezi.
Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper wakifurahia jambo.
KISA MSONGO WA MAWAZO
Uchunguzi wa Risasi Jumamosi umebaini kwamba, mastaa hao wana msongo wa mawazo hivyo wanaona njia pekee ya kuwaondolea ‘stresi’ ni kunywa pombe.
WEMA
Habari za ndani zilieleza kwamba, tangu Wema ameachana na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekuwa mtu mwenye mawazo na njia pekee ambayo huitumia ni kujipooza kwa pombe kali.
“Ndiyo maana ana mpaka kaunta ya pombe kali nyumbani kwake,” alisema mmoja wa watu wake wa karibu (Team Wema).
ZARI ATAJWA
Ilisemekana kwamba mbali na mawazo ya Diamond ambaye amehamia kwenye nyumba ambayo Wema alikuwa na mchango mkubwa wakati wa ujenzi, pia suala la jamaa huyo kutanua na mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’ limekuwa likimpa wakati mgumu mwanadada huyo.
Staa katika tasnia ya filamu, Bongo Wema Isaac Sepetu.
SUALA LA UGUMBA
Habari zilieleza kuwa, jambo lingine linalompa Wema msongo wa mawazo ni suala la kukosa mtoto kila anapomtafuta akiamini kuwa watu wanajua yeye ni mgumba.Pia ilielezwa kwamba kuna suala la kuishiwa na kuogopa kufilisika kwani kwa sasa filamu hazilipi na bado anataka kuendelea kuwa na heshima ya kuitwa Madam hivyo njia pekee anayoona inafaa kutuliza mawazo ni kunywa pombe.
WOLPER
Kwa upande wake Wolper uchunguzi ulionesha kwamba, kwanza anapenda fedha hivyo kukosa tenda za kuigiza na kuanguka kwa soko la filamu za Kibongo kumemsababishia msongo wa mawazo kama ilivyo kwa Wema kwani naye anataka kuishi maisha ya kistaa ambayo hayawezekani bila kuwa na mshiko.
WOLPER KALOGWA?
Akizungumzia hali hiyo, Wolper alikiri kuwa na mawazo mengi huku akihisi kuwa huenda amelogwa.
USHAURI WA KISAIKOLOJIA
Staa katika tasnia ya filamu, Bongo Jackline Wolper.
Kwa mujibu wa mtaalam wa saikolojia aliyezungumza na gazeti hili juu ya mastaa aliwashauri kama ifuatavyo;
Mtaalam huyo alishauri mastaa hao kuachana na pombe na kama wana mawazo ya kuumiza, wanatakiwa kujilazimisha kutabasamu mara kwa mara na kusahau jambo linalowaletea mawazo mabaya.
Alisema kuwa, kutabasamu kutawasaidia kuchangamsha akili, ingawa inaweza kuchukua muda kurudi katika hali ya kawaida lakini inasaidia kuamsha hisia za furaha zilizokuwa zimeshambuliwa na mawazo mabaya na kuamini katika ushindi.
WASISAHAU NYUMBA ZA IBADA
Pia aliwashauri kusahau mambo yaliyopita na kujikita katika kufanya kazi kwa bidii hata kama matunda hawayaoni sasa, yatakuja baadaye.Mbali na hivyo wajitahidi kujichanganya katika makundi ya watu sahihi na kujumuika kwenye nyumba za ibada, msikitini (kwa muislam) na kanisani (kwa mkristo)


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Msangi.
MSHITUKO wa matukio ya mfululizo ya ajali, umeendelea kugubika nchi, baada ya watu 20 kupoteza maisha katika ajali ya basi dogo aina ya Toyota Hiace, iliyotokea jana wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
Ajali hiyo ambayo taarifa na picha zake zilisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, imesababisha taharuki kutokana na ukaribu wake na matukio mengine ya ajali yaliyotokea wiki hii.
Baadhi ya wakazi wa jirani na eneola tukio wakitazama gari lilivyopata ajali kando kando ya mto Kiwira.
Tangu Jumapili iliyopita mpaka jana, siku zisizozidi sita kumetokea ajali kubwa tatu zilizohusisha mabasi ya abiria na kuteketeza maisha ya watu 40.
Mbali na ajali hizo, wiki hii Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alitoa takwimu zilizosababisha huzuni kwa Watanzania, kwamba kati ya Januari mosi na Aprili 12 sawa na siku 102, watu 969 walipoteza maisha katika ajali za barabarani.
Wananchi wa Kiwira wakiangalia baadhi ya Miili ya Watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Ajali za wiki
Jumatano wiki hii, basi la Air Jordan lililokuwa likitokea mkoani Mwanza kwenda Arusha, lilipata ajali na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi 20.
Ajali hiyo ilitokea wakati Watanzania wakiwa na kumbukumbu ya ajali iliyotokea Jumapili ya wiki jana, ambapo watu 19 waliteketea kwa moto, baada ya basi la Kampuni ya Nganga Express na lori aina ya Fuso kugongana uso kwa uso na kuwaka moto katika eneo la Iyovi, Milima ya Udzungwa, mkoani Morogoro.
Ajali ya Mbeya
Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Msangi, alisema ajali hiyo mpya imetokea katika eneo la Ilongo ambalo limebatizwa jina la Uwanja wa Ndege karibu na Kiwira, ambapo watu 18 walipoteza maisha papo hapo.
“Watu wanne waliojeruhiwa, mmoja alikuwa katika hali mbaya na kwa bahati mbaya alifia njiani wakati akipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe kwa matibabu,” alisema Kamanda Msangi.
Kamanda Msangi alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na dereva kutokuwa makini katika uendeshaji wake. Taarifa zilizotufikia baadae, zilieleza kuwa abiria mwingine aliyekuwa akipatiwa matibabu, alifariki akiwa hospitalini.
Mashuhuda
Mashuhuda wa ajali hiyo walidai kuwa chanzo cha ajali ni mwendokasi uliosababisha dereva ashindwe kumudu gari hilo katika mteremko wenye kona, akajikuta gari likimshinda na kutumbukia katika Mto Kiwira.
Walidai kuna uwezekano dereva huyo alikuwa akikimbizwa na baadhi ya madereva wa mabasi aina ya Toyota Coaster, yanayofanya safari zake kati ya Mbeya, Tukuyu na Kyela.
Musa mateja
KIAPO! Kuonesha kwamba hana mpango wa kurudi nyuma, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ amefungukia msimamo wake juu ya mwandani wake wa zamani, Wema Sepetu ‘Madam’ kwa kusema kuwa kamwe hawezi kumrudia tena, Risasi Jumamosi lina mkanda kamili.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.
Licha ya Diamond kufunguka hayo, wawili hao wamekuwa na mapenzi ya vipindi, kuna wakati waliwahi kumwagana kisha kurudiana na hakuna aliyewahi kutoa tamko zito lakini safari hii Diamond amesema ndiyo basi tena!
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na staa huyo, mara kwa mara Diamond amekuwa akijiwekea nadhiri ndani ya moyo wake na kusisitiza kwamba pamoja na kuwa maisha ya sasa huendeshwa kwa msingi wa fedha lakini hata kama ‘atafulia’ kiasi gani, ni bora afe maskini kuliko kurudiana na Wema.
“Diamond amekuwa akisema kila wakati kwa msisitizo kuwa kutokana na matatizo aliyokumbana nayo katika uhusiano wake kwa Wema, ni vigumu sana kurudiana naye wala kuwaza kama ipo siku anaweza kuwa naye, maana hakuna tena jambo geni asilolijua kwake,” kilisema chanzo hicho na kufunguka zaidi:
“Kama hiyo haitoshi, Diamond anasema anaposema haoni kitu kipya  kwa Wema anamaanisha ndiyo maana utaona leo hakuna hata siku moja ambayo amewahi kuwaza kurudiana naye hata kama atatumia ushawishi wa fedha kwa kumpelekea makontena ya fedha, hawezi kukubali anasema bora afe maskini kuliko kushea kitanda kimoja na Wema.”
DIAMOND ATHIBITISHA
Baada ya madai hayo, Risasi Jumamosi lilifanya jitihada za kukutana na Diamond uso kwa uso ambaye alithibitisha taarifa ambazo zilielezwa na mtu wake wa karibu:
“Umeambiwa na nani hayo? Sipendi kuongelea sana hivi vitu lakini huo uliousikia ndiyo ukweli. Kwa sasa nawaza maisha yangu na mpenzi wangu Zari baada ya kupitia majaribu mengi kimapenzi enzi hizo.
“Huenda wengi wasiamini ninayosema lakini nafsi yangu haijawahi kuniongoza kukumbuka ya nyuma tena kama ilivyowahi kutokea awali.
“Wengi wamekuwa wakiniuliza swali kama hili lakini sikupenda kujibu kwa kuwa nilihisi litaleta tafrani kwa mashabiki wangu, sioni sababu ya kuendelea kuulizwa kwenye media hivyo ukweli ni kwamba siwezi kurudi nyuma tena,” alisema Diamond.
Wema Sepetu ‘Madam’.
ASISITIZA KWA KUREKODI WIMBO
Kuonesha kweli amedhamiria kutogeuka nyuma, Diamond alisema kwa sasa yuko bize studio kurekodi wimbo na Nay wa Mitego (Emmanuel Elibariki) ambao utakuwa umesheheni majibu ya maswali yote ya kila kitu ambacho kilimkera kwenye uhusiano wake na Wema.“Naomba mashabiki wangu wawe na subira kwa maswali hayo yote, majibu yake yatapatikana katika project yangu na Nay inayokuja muda si mrefu,” alisema Diamond.
WEMA AJIBU MASHAMBULIZI
Alipotafutwa Wema kuhusiana na kauli hiyo ya Diamond, naye alijibu mashambulizi kwa kusema kamwe hawezi kurudiana na Diamond, hamfai hata kidogo na hata akimshawishi na  fedha nyingi kiasi gani hawezi kurudi nyuma.
“Hata aje na Bill Gates (tajiri mkubwa duniani), aje na matajiri wote anaowajua yeye duniani kamwe siwezi kulamba matapishi, kwanza sitaki kukumbuka kabisa kuhusu huyo mtu, please naomba nisimuongelee kabisa huyo mtu,” alibwatuka Wema.
WAMEFIKAJE HAPA?
Wawili hao ambao walidumu kwenye uhusiano na kupamba vyombo mbalimbali vya habari, kila mmoja amekuwa akimtuhumu mwenzake kuwa msaliti lakini sababu kubwa ambayo Diamond amekuwa akiisimamia juu ya kummwaga Wema ni baada ya mrembo huyo kuhongwa gari na mwanaume mwingine.
Waandishi wetu
MTOTO mzuri ndani ya anga la Bongo Fleva, Esterlinah Sanga ‘Linnah’ amezua gumzo la aina yake baada ya kutupia picha yake mtandaoni akiwa ametinga mavazi mafupi yaliyoacha sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi.
Mtoto mzuri ndani ya anga la Bongo Fleva, Esterlinah Sanga ‘Linnah’.
Linnah alitupia picha hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram hivi karibuni na kuwafanya watu wengi wanaotumia mtandao huo kusambaziana picha hivyo huku kila mmoja akiibua maswali yake.Haya ni baadhi ya maoni ya watu tofauti kuhusiana na picha hiyo: ‘Mh! Hii amezidisha sasa Linnah jamani’, ‘amependeza msimfanyie hivyo mtoto wa watu’, ‘mzuri ni mzuri tu hata avae gunia, big up Linnah’
Mabasi yaendayo mikoani yakiwa Stendi ya Ubungo yamepaki.
Wasafiri wakiwa hawajui hatma ya safari yao eneo la Ubungo.
Hali halisi ya Ubungo ilivyokuwa asubuhi leo.
Muonekano wa eneo la Ubungo-Darajani hali ilivyokuwa.
Kituo cha daladala cha Shekilango hali ilivyokuwa.
Umati wa watu ukimshuhudia jamaa mmoja aliyekuwa akitoa ibada fupi ya kuombea nchi kuhusiana na mgomo wa madereva ambao ni wa nchi nzima eneo la Ubungo.
Usafiri wa bodaboda ukionekana kufanya kazi bila kugoma.
Madereva wa Bajaj nao wakipakia abiria maeneo ya Ubungo jijini Dar.Abiria wakitafakari kuhusu safari yao.
MADEREVA wa mabasi ya mikoani na daladala wa jijini Dar leo wamefanya mgomo kupinga agizo la Mamlaka ya Kudhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) lililowataka kwenda kusoma katika Chuo cha Usafirishaji (NIT).
Mwandishi wetu amezunguka maeneo tofautitofauti jijini Dar na kujionea hali halisi ya mgomo wa mabasi ya mikoani pamoja na daladala za maeneo tofauti ya Jiji la Dar.
Mwandishi wetu pia aliweza kufika eneo la Stendi ya Ubungo na kujionea hali ilivyokuwa asubuhi na kuzungumza na baadhi ya madereva ambao walikuwa na kauli tofautitofati kuhusiana na mgomo huo.
Mmoja wa madereva ambaye alijitambulisha kwa jina la Ally Abdallah Shalon anayefanya kazi zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma, alisema kuwa sababu kubwa ya kutokufanya shughuli zake ni kutokana na kikao ambacho walipanga kukifanya leo kujadili agizo la Sumatra lililowataka waende shule kusoma.
Dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Khamis anayefanya shughuli zake kati ya Mwanza na Dar es Salaam alisema sababu iliyomfanya agome ni kupinga sheria mpya ya Sumatra iliyopitishwa na jeshi la polisi kuwataka madereva wote wa abiria (Pasangers Services Vehicle) kwenda kusoma kozi ya miezi miwili kwa gharama ya shilingi laki tano.
Khamisi alisema sheria hiyo inawabana sana madereva kwani moja kati ya vipengele vya sheria hiyo imeeleza kuwa, dereva yeyote atakayekamatwa akiwa amezidisha mwendo kasi hakuna faini yoyote bali unapelekwa mahabusu kwa muda wa siku kumi na nne baada ya kumaliza siku hizo, anapelekwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
“Hii sheria inatubana sana, mtu ukihitaji kubadilisha leseni yako ikipitwa na muda unatakiwa kurudia tena kwenda kusoma darasani kwa muda wa wiki mbili kwa ada isiyopungua laki tano na kuendelea kitu ambacho kinatuumiza sisi madereva,” alisema Khamis.
MUSOMA
Huko Musoma, abiria zaidi 1000 waliokuwa wakisafiri kutoka Musoma kwenda Dar es Salaam kupitia mkoani Mwanza na Shinyanga na wale wa kwenda mpakani mwa Tanzania na Kenya pamoja na wa ndani ya Mkoa wa Mara wameshindwa kusafiri baada ya madareva kuitisha mgomo leo.
KIBAHA
Zaidi ya mabasi 10 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa yamekwama huko Kibaha mkoani Pwani kutokana na mgomo wa madereva leo.
BUKOBA
Mabasi yote ya abiria yaliyotoka Bukoba Mjini leo asubuhi kuelekea Dar, Mwanza na kwingineko yamezuiliwa wilayani Muleba kutokana na mgomo wa madereva unaoendelea nchini kote. Abiria wamerudi mjini Bukoba kurudishiwa nauli zao na kuahirisha safari
Previous PostOlder Posts Home