MUME WANGU SIKUMUIBA KWA RAFIKI YANGU- VANITHA

WANGU SIKUMUIBA KWA RAFIKI YANGU- VANITHA




Wiki hii kupitia safu hii tunaye staa wa filamu za Kibongo Vanitha Omary. Amebanwa maswali mengi na mwandishi wetu Hamida Hassan lakini kutokana na jina la kolamu hii, tunakuletea maswali 10 ‘hot’ aliyoulizwa na yeye kutoa ushirikiano katika kuyajibu licha ya kwamba aliachwa kijasho chembamba kikimtoka.
Staa wa filamu za Kibongo Vanitha Omary.
Ijumaa: Kuna hizi tetesi kwamba huyu mume wako wa sasa alikuwa ni mpenzi wa rafiki yako Joan Matovolwa lakini wewe ukampora na mkaishia kuoana, hili unalizungumziaje? Vanitha: (Kicheko) Ukweli ni kwamba mimi na Joan ni marafiki wakubwa na hilo unaloongea halina ukweli wowote. Maneno hayo yaliibuka baada ya kuwepo taarifa kuwa nataka kuolewa.
Ijumaa: Wewe ni msanii lakini ni mke wa mtu, siku ukiwa hujaenda kwenye shughuli zako za kisanii uwapo nyumbani huwa unafanya nini? Vanitha: Huwa napenda kupikapika. Wewe ni mke wa mtu halafu ni sanii, je unapokuwa nyumbani unapenda kumpikia chakula gani mumeo?
Vanitha: Nikiwa nyumbani napenda kumpikia baby wangu chakula kizuri ambacho ni kipya. Ijumaa: Je, pale unapokuwa faragha na mumeo unapenda kumtega kwa vivazi gani?Vanitha: Ukweli huwa simtegi kwa mavazi, napenda kumtega kwa kukaa mtupu kwani wakati huo huwa ni wake, kwa nini nimfichie mali zake?
Ijumaa: Ni upi ugonjwa wako uwapo faragha na huyo mumeo?
Vanitha: Napenda sana kumkumbatia na yeye anikumbatie. Kale kajoto kanakotokea huku tukinong’onezana maneno matamu mimi nabaki kusinziasinzia.
Ijumaa: Watu wanasema wanaume hawatabiriki kwa kuchepuka, hivi siku ukimfumania mumeo utafanya nini?Vanitha: Naomba Mungu isitokee kwani nahisi nitafanya tukio baya na kumuacha siwezi, dah! Nahisi kutetemeka ukiniambia hivyo



Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment