AFARIKI AKIFANYA MASIHARA MTONI

Marehemu Jackson Nyambele enzi za uhai wake.
WAANDISHI wetu
KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Jackson Nyambele (28) mkazi wa Mbezi Mtoni jijini Dar, amefariki dunia baada ya kusombwa na maji ya mto uliopo Mbezi alipokuwa akifanya masihara na wenzake.Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Machi 22, mwaka huu ambapo chanzo chetu makini kinadai kuwa, awali marehemu alikuwa akibishana na wenzake kwamba yeye anaweza kuvuka kwenye mto huo mwingine akiweka dau kuwa, atakayeweza kuvuka atampa pesa.
Mamaake akilia kwa simanzi kubwa wakati wa kuaga.
“Walipokuwa wakibishana kuhusu kuvuka mto ule na mwenzao mmoja kuahidi kuwa atakayevuka atapewa fedha, ghafla sehemu ya udongo aliokuwa amekanyaga Jackson ulimomonyoka na kumfanya ateleze na kutumbukia mtoni.
Ndugu jamaa na marafiki wakiaga mwili wa marehemu.
“Hakuna aliyeweza kumsaidia kwa sababu maji yalikuwa mengi na ya kasi sana huku yakiwa na matakataka kiasi kwamba hata kama unaweza kuogelea, ni vigumu kuyamudu,’’ kilidai chanzo hicho.
Ikaelezwa kuwa, baada ya kufuatiliwa ndipo mwili wake ukakutwa ufukweni mwa bahari huko Kunduchi ukiwa umejaa maji.
Mwili ukiandaliwa kwa ajili ya mazishi.
Akizungumza na waandishi wetu, Mwenyekiti wa Mtaa anaoishi Jackson, Rehema Muya alisema tukio hilo ni la kusikitisha na mto huo miaka ya hivi karibuni umeua watu wapatao 10 katika mazingira ya kutatanisha.
Mwili wa marehemu Jackson umezikwa Jumanne iliyopita katika makaburi ya Mbezi Juu. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amen.
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment