Hakuna kitu kizuri kama kumwambia mpenzi wako ‘umependeza’ pale anapokuwa amependeza. Kauli hiyo itamfanya ajione thamani yake. Itamfanya ajue kwamba ili uweze kumwambia amependeza, anatakiwa avae mavazi ya aina gani.
Asikwambie mtu, hakuna mtu ambaye hapendi kuambiwa amependeza hususan wanawake. Hivyo basi, ukiona mwenzako amependeza pindi unapokutana naye, hilo liwe suala la kwanza kumsifia kwamba amependeza.
Ikiwezekana kama kuna vazi ambalo unaona ni zuri na unaamini mwenzako akilivaa litampendeza, mnunulie au ikiwezekana mshauri avae vazi la namna hiyo. Jukumu la kujua amependeza linakuhusu wewe kama mwenza wako na si mtu mwingine yeyote.

KUJALI AFYA
Kwa wapendanao kila mmoja ana wajibu wa kumjali mwenzake kuhusu afya. Mwenzako akiwa anaumwa, wewe ndiyo uwe wa kwanza kumjulia afya na kutoa ushauri wowote ambao utasaidia kumfanya mpenzi wako arudi katika hali ya kawaida.

Mtie moyo kwamba ugonjwa anaoumwa ni wa kawaida, kuwa naye karibu kwa kumuuliza ‘unaendeleaje? Unajisikiaje?’ Hili suala ni muhimu sana husasan kwa wanaume, wanaume wengi wana kasumba ya kutojali wanawake wao hivyo ni vyema nao wakabadilika.
Kumuuliza mtu unaendeleaje si kwamba ndiyo atapona lakini unapofanya hivyo unaongeza faraja kwa mgonjwa. Unampa nguvu maana wewe ndiye mtu wake wa karibu zaidi, ndiye msiri wake.
MTOKO
Suala la mtoko mara nyingi limezoeleka kwa wanaume kuwatoa wanawake lakini kimsingi siyo sheria. Mwanamke pia anaweza kumtoa ‘out’ mwenzake. Si lazima umtoe mwenzako muende katika sehemu ambayo itakuwa ya gharama kubwa, unaweza kumtoa mkaenda ufukweni tu akatazama mandhari ya bahari.

JALI NDUGU ZAKE
Hii pia inasaidia. Mnapokuwa wapenzi kila mtu anakuwa na ndugu zake. Anapokueleza kwamba kuna tatizo katika upande wake, onesha kwamba unajali hata kama huna uwezo wa kulitatua. Uwe wa kwanza kumuuliza, fulani anaendeleaje siyo hadi akwambie yeye kwamba fulani anaendelea vizuri.

Toa ushauri juu ya ndugu wa mwenzako pale unapoona una uelewa wa kitu fulani, siyo lazima utoe fedha lakini ushauri wako unaweza kutoa suluhisho ambalo hata wewe mwenyewe hukulitarajia. Kuulizia hali ni kitu kidogo lakini kina maana kubwa tu.
MADHARA
Endapo hautavifanya hivyo vitu ambavyo unaweza kuona ni vya kipuuzi, madhara makubwa yanayoweza kutokea katika penzi lenu au ndoa, ni kutawaliwa na migogoro ya kila kukicha. Japo ni vitu vidogo lakini vinaweza kusababisha mkaachana.

Ni rahisi mwenza wako kupata mtu mwingine ambaye anaweza kumfanyia vitu hivyo na kukuona wewe huna umuhimu kwake. Ataanzisha uhusiano na yule anayemfanyia vitu hivyo, matokeo yake penzi lenu litakuwa limeingia dosari pasipo wewe kujua.
Kama unaamini ni vitu vidogo, havikupunguzii kitu katika mawazo wala nguvu zako, vifanye ili visisababishe penzi lenu likavunjika.Kwa leo tuishie hapo, tukutane tena wiki iajyo kwa mada nyingine nzuri.
0 comments:
Post a Comment