Dustan Shekidele, Morogoro
Kazi ipo! Mwandani wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ juzikati alizua kizaazaa kisa ujauzito alipohudhuria kwenye msiba wa aliyekuwa bosi wa Tip Top Connection, Abdul Taletale ‘Abdul Bonge’ aliyefariki dunia ghafla wikiendi iliyopita.
Mwandani wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari akifichwa na bodigadi wake.
Tukio hilo la Zari lilichukua nafasi katika Kijiji cha Mkuyuni, Tarafa ya Matombo mkoani hapa ambapo mastaa kibao walisafiri kutoka Dar kwa ajili ya mazishi ya kiongozi huyo.
ILIKUWAJE?
Awali, katika tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa mapema Jumanne wiki hii, Zari na Diamond, wakiwa wameongozana na wapambe wao walifika eneo la msiba ambapo kwa taratibu za Kiislam, wanawake hawachanganyiki na wanaume hivyo Zari akachukuliwa kwenda upande mwingine huku Diamond akielekea upande wa wanaume.
HALI YA HEWA YABADILIKA
Mara baada ya mastaa hao kutinga eneo hilo, umati mkubwa uliokuwa msibani hapo ulianza kuwazingira huku kila mmoja akitaka kuwaona.Akiingizwa garini.
ZARI AIBUA KIZAAZAA
Akiwa upande wa wanawake wenzake, Zari alijikuta akizungukwa na baadhi ya watu walionekana wazi kumchunguza kuanzia miguuni hadi kichwani ikidaiwa kuwa, walikuwa wakicheki kama kweli ana mimba ya Diamond.
“Mwee, huyu ndiye Zari wa Diamond! Hivi mimba anayo kweli au ndiyo haya mambo ya mastaa wetu, mhh lakini kweli kitumbo kama kimetuna vile,” alisikika akisema mmoja wa wanawake hao.Uwepo wa mwanadada huyo uliwafanya wengi kusahau ishu ya msiba na kujikuta wakipigana vikumbo kumshangaa Zari ambaye muda mwingi alikuwa akijificha.
Kutokana na mazingira ya watu kukanyagana kutaka kumuona staa huyo, mrembo aliyefahamika kwa jina la Jestina George aligeuka kuwa bodigadi wake ili kumuepushia usumbufu ambapo alifanya kazi ya kumlinda.
PAPARAZI AZUIWA KUMPIGA PICHA
Paparazi wetu aliyekuwa eneo la msiba kwa lengo la kupata picha za kumbukumbu kwamba Zari aliwahi kufika eneo hilo, alikumbana na wakati mgumu baada ya Jestina kumpiga mkwara asijaribu kupiga picha.
 “Weee, ukijaribu kupiga picha tunakorofishana, mwenyewe hataki kupiga picha, kama vipi nenda kamuombe ruhusa Diamond,” alisema Jestina huku akimficha Zari.Diamond akiimalisha usalama kwa mpenzi wake.
WATU WAANZA ZOGO
Kufuatia kitendo cha Jestina kumzuia mwandishi wetu kupiga picha, zogo lilianza eneo hilo huku baadhi ya watu wakihoji sababu za Zari kufichwa.“Au ni hiyo mimba yake ndiyo maana hamtaki apigwe picha? Acheni hizo bwana,” alisikika akiwaka kijana mmoja.
PAPARAZI AMFUATA DIAMOND
Baada ya paparazi kupigwa mkwara asipige picha alilazimika kwenda kumtafuta Diamond ili ampe ruhusa ya kwenda kumfotoa Zari lakini staa huyo naye alikataa na kueleza kuwa, kama anataka kufanya hivyo akachukue ruhusa kutoka kwa meneja wake.
Meneje huyo wa Diamond aliyefahamika kwa jina moja la Salam alipofuatwa alimruhusu paparazi kufanya kazi yake lakini aliporudi nyumbani palipokuwa na msiba kwa nia ya kumfotoa Zari, hali ilikuwa ileile hivyo kumsubiria mpaka Diamond alipotoka makaburini na alipofika kwenye gari lao, Zari alitolewa kwa kufichwa na Jestina kiasi cha kuwepo ugumu kupata sura yake.
ZARI AINGIA KWENYE GARI FASTA
Huku watu wakimfuata kwa nyuma, Jestina alimchukua Zari na kumficha kwapani kisha kumkimbizia kwenye gari tayari kwa kuondoka eneo hilo.
DIAMOND NAYE APATA WAKATI MGUMU
Wakati Diamond akirejea kutoka makaburini, alijikuta akizingirwa na baadhi ya vijana ambao wengi wao hawajawahi kumuona ‘live’ hivyo kumpa wakati mgumu.Hata hivyo, ili kuwafurahisha, vijana hao walipata fursa ya kupiga naye stori mbili-tatu kabla ya kuondoka eneo hilo na kuacha umati ukiwasindikiza kwa macho.

Sasabo Steven
MSANII wa muziki wa Hip Hop Bongo, Erick Msodoki ‘Young Killer’ amekanusha madai kuwa demu wake anayejulikana kwa jina la Halimaty ana miaka chini ya 18.Akipiga stori na Ijumaa kuhusiana na ishu hiyo, Young Killer anashangaa watu kudai demu wake huyo ni ‘under age’ wakati ukweli ana miaka 20.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Erick Msodoki ‘Young Killer’ akiwa na demu wake.
“Mpenzi wangu ana miaka 20 na siyo kwamba eti nimemchukua kihuni tu mtaani, hapana! Nimempata kwa ridhaa ya wazazi wake sasa nashangaa hizo tuhuma zinatokea wapi,” alisema Young Killer

Na Waandishi Wetu
Imejulikana kwamba kilichomponza Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (pichani) pamoja na madai ya kutumia maneno yenye kuudhi kwa Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycap Kadinali Pengo mambo ya kisiasa yametajwa kuwa ndiyo msingi wa kushughulikiwa kwake.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Gwajima anadaiwa kushabikia upande mmoja wa kisiasa katika mbio za urais, mwaka huu, huku Kadinali Pengo naye akihusishwa na ufuasi wa upande mwingine.Kikizungumza na Gazeti la Uwazi juzi, chanzo chetu kimoja kilisema kuwa, katika maneno yake ya kumshambulia Kadinali Pengo, Gwajima alisema anaamini Pengo aliyageuka makubaliano ya maaskofu wenzake kwa sababu anamuunga mkono mgombea mmoja wa urais mwaka huu.
“Lakini sasa nawaambia kwamba, hata Gwajima mwenyewe kilichomfanya akazungumza vile ni yeye kuwa upande wa mgombea mmoja wa urais (hamtaji).“Yaani yeye alimsema mwenzake (Pengo) kwamba ametumwa na mgombea mmoja, lakini na yeye pia anatumika kisiasa na mgombea mwingine.
“Ishu ya Gwajima hakuna kingine, ni mnyukano wa kambi za kisiasa (chanzo hakifafanui kambi hizo) na hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu. Maaskofu walikaa wakakubaliana kuwaambia waumini wao wasipigie kura Katiba Inayopendekezwa kwa sababu ya hoja ya Mahakama ya Kadhi, Kadinali Pengo akaja kutoa tamko peke yake kwamba, waumini waachwe waamue wenyewe.
“Pengine Pengo ana mlengo wake ili katiba ipite kwa manufaa fulani, lakini Gwajima naye aliamua kufanya vile kwa sababu anasimamia masilahi ya kundi lake,” kilisema chanzo chetu.Kikaendelea: “Kwa hiyo jamani kama si siasa, Gwajima asingeyasema yale maneno makali vile. Naye alikuwa kazini.”
Gwajima kumnenea maneno yenye kuudhi Kadinali Pengo ndiyo habari ya mjini kwa sasa ambapo, wiki iliyopita, mchungaji huyo alijisalimisha polisi baada ya kutakiwa kufanya hivyo na jeshi hilo.Hata hivyo, wakati Gwajima akihojiwa, ghafla alisikia kizunguzungu na kuanguka ambapo alikimbizwa katika Hospitali Polisi Baracks kisha Hospitali ya TMJ, Dar kwa matibabu zaidi.
Wakati  akiendelea na matibabu, inadaiwa juzi usiku wa manane watu 15 walikamatwa kwa madai ya kuonesha mazingira ya kutaka kumtorosha mchungaji huyo.Watu hao walidakwa wakiwa na begi moja la nguo, huku duru za usalama zikidai kuwakuta pia na silaha (bastola) na hati ya kusafiria.
Akizungumza katika mahubiri ya kanisa hilo juzi katika Kanisa la Gwajima lililopo Kawe, Dar, mchungaji mmoja (jina halikupatikana mara moja) alisema kuwa, watu waliokamatwa hawakuwa na lengo baya kwani walikwenda kumpelekea Gwajima nguo za kuvaa. Silaha ilikuwa ndani ya begi, Gwajima anaimiliki kihalali, ingawa hoja inabaki kuwa kwa nini wampelekee nguo za kuvaa usiku wa manane


Na Haruni Sachawa
NImaajabu! Mwanamke mmoja, Diana Dioniz  mkazi wa Magomeni Makuti jijini Dar es Salaam, ameangua kilio cha kuomba msaada baada ya mtoto wake aliyezaliwa mwaka mmoja uliopita kugundulika kuwa hana ubongo wa nyuma (medulla oblongata), hali inayosababisha shingo kulegea na macho kutoona.
Mtoto anayedaiwa kuzaliwa bila ya ubongo wa nyuma(medulla oblongata).
Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake, Diana alisema alipata ujauzito wa mtoto huyo na kujikuta akiwa na furaha kubwa, lakini baada ya kuzaliwa na kumpa jina la John, amejikuta akipata mateso makubwa, kwani kwa muda wote, shingo yake inakuwa imelegea na macho yake hayaoni.
“Majirani walinishauri nimpeleke hospitali kwa uangalizi zaidi, nilipomfikisha Muhimbili nikaambiwa suala la mwanangu linapaswa kushughulikiwa na daktari bingwa wa magonjwa ya watoto wa Kitengo cha Moi,” alisema mwanamke huyo.
Aliongeza kuwa, baada ya kupelekwa huko na kuchunguzwa ndipo ilipojulikana kuwa na matatizo hayo, ambayo yamemfanya kuwa na wakati mgumu katika kumlea, kwani analazimika kuwa naye karibu kwa muda wote, jambo linalomfanya kukosa muda wa kufanya majukumu mengine.
Mtoto huyo akiwa na mamayake.
“Hali yangu ya kimaisha ni ngumu sana, sina msaada wowote hapa, nakaa kwa bibi mzaa baba, mama yangu yuko kwao, kwa sababu walishaachana na baba yangu  muda mrefu na kwa sasa  baba ana familia kubwa huko Mwanza.
“Ninawaomba Watanzania wanisaidie ili mtoto aweze kukaa, pia naomba pesa kwa ajili ya kumhudumia kupata  maziwa na matumizi mengine kama kiti cha magurudumu (wheelchair). Aliyeguswa na habari hii awasiliane nami kwa simu namba 0718 690219,” alisema Diana.

NIANZE kwa kutoa pole kwa wadau wote wa muziki wa kizazi kipya, kwa kuondokewa na mdau Abdul Bonge, muanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection, wale vijana wenye maskani yao pale Manzese.
Bonge ametutoka katika wakati ambao Bongo Fleva ndiyo ilikuwa inamhitaji zaidi, kwani hakuna ubishi kwamba muziki huu sasa unalazimisha njia kuelekea nje ya nchi na hawa ndiyo walikuwa wawezeshaji wakuu wa jambo hili. Mungu ampe mapumziko mema peponi na tumuahidi tu kuwa nasi tupo njiani, tutakutana naye muda na wakati wowote kuanzia sasa!
Baada ya pole hiyo, kwa wasanii, wadau na jamii yote, sasa nirejee kwenye mada yangu ambayo nazungumza na staa wa Bongo Fleva aliye katika levo za juu kabisa, Diamond Platnumz.
Hivi karibuni kulikuwa na habari zilizosema kuwa msanii huyo amehamia katika nyumba yake ya bei mbaya aliyoijenga huko Madale, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kabla ya kuhamia, kama walivyo vijana wengi wa sasa, ‘alitupia’ picha kadhaa katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram akionyesha sehemu mbalimbali za nyumba hiyo ya kisasa.
Alionyesha bwawa la kuogelea, samani zilizopo sebuleni na jikoni kwake sambamba na vitu vingine vilivyoendana na jumba lake hilo. Lakini katika hali ya kushangaza, siku chache baadaye alisikika akisema kutokana na ukubwa na thamani ya nyumba yake, vinamfanya ahofie maisha yake, hasa nyakati za usiku anaporejea kutoka kazini au matembezini (Wasanii mara nyingi hufanya kazi usiku).
Kwanza nimpongeze sana Diamond kwa kufanikiwa kumalizia nyumba yake maana vijana wengi wa umri wake, bado wanaishi kwa wazazi wao. Lakini wakati nikimpongeza, napenda pia kumshauri kuwa hivi sasa ameshakua mkubwa, siyo tu kiumri, bali hata kiakili, kiasi kwamba anapaswa kuacha kufanya baadhi ya mambo ambayo kimsingi, yanapishana naye.
Hatari anayoihisi kule nyumbani kwake alikojenga, ameitengeneza mwenyewe. Ujana na ukisasa, unamfanya kuweka picha za baadhi ya vitu vilivyomo ndani ya nyumba yake, jambo ambalo siyo baya, lakini unapoishi na jamii iliyokata tamaa kama yetu, siyo jambo zuri.
Nchi yetu ina vijana wengi wasio na ajira, ambao wamekosa fursa na bahati mbaya, wengi wao hawana elimu ya kutosha. Matokeo yake wanaishi kwa kubangaiza ilimradi siku zinakwenda. Wakati Diamond ana uwezo wa kujenga nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 400, wenzake wengi hawana hata uhakika wa mlo wa siku.
Aina ya maisha ya Diamond, yanashawishi watu kudhani ni tajiri sana, mwenye uwezo mkubwa kimaisha na hivyo ni kijana anayenuka fedha. Kama nilivyosema, anaweza kuwa ni shabiki wa wengi, lakini unapofikiria kuhusu tabu za maisha, watu hawaoni hatari kumdhuru ilimradi kama wana uhakika kuwa watapata kitu cha kuwapunguzia ukali wa maisha.
Nadhani huu ni wakati wa Diamond kupunguza maisha ya video. Ni haki yake kuamua chochote kinachomhusu, lakini busara haishawishi mtu kutangaza unachomiliki pasipo sababu za msingi. Binafsi ninawajua wasanii wengi ambao ‘wako vizuri’ kimaisha, lakini huwezi kuwadhania ukiwaona.
Yapo baadhi ya mambo tunayafanya kwa sababu ya umri, ambayo kadiri tunavyokua hatuwezi kufanya. Wabongo hawajui kuwa unaweza kuwa na nyumba kubwa, lakini usiwe na fedha ndani, watakuja na mapanga yao kulazimisha uwape fedha, wasipopata utaambulia majeraha.
Ni kweli hata mastaa wa Ulaya wanaanika wanachomiliki, lakini tambua kuwa ipo tofauti kubwa kati yetu. Wewe bado ni kijana mwenye ndoto nyingi, acha matangazo, timiza ndoto zako!

Na Elvan Stambuli
‘SARAKASI’ za Mkutano wa 19 wa Bunge la 10 zitaanza leo mjini Dodoma na imeelezwa kuwa ni maalum kwa ajili ya kushughulikia miswada ya sheria ikiwemo Sheria ya Makosa ya Mtandao (The Computer and Cyber Crimes Bill, 2015) na ya vyombo vya habari ambazo tayari zimetinga bungeni.
Bunge la jamhuli ya muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa ya Bunge, jumla ya miswada sita itawasilishwa bungeni kwa Hati ya Dharura na inakusudiwa kupitishwa katika hatua zake zote.
Pamoja na Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, mingine ni Muswada wa Sheria ya Kupata Habari wa Mwaka 2015 (The Access to Information Bill, 2015), Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari wa Mwaka 2015 (The Media Services  Bill, 2015) na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa Mwaka 2015 (The Fair Competition Amendment Bill, 2015).   
Miswada mingine ni  Muswada wa Sheria ya Miamala ya Kielektroniki wa Mwaka 2015 (The Electronic Transaction Bill, 2015) na  Muswada wa Sheria ya Gesi Asilia wa Mwaka 2015 (The Natural Gas Bill, 2015).
Kuja kwa miswada ya habari kunaweza kuwa ‘ukombozi’ kwa wana habari kwani wamekuwa wakiilalamikia serikali, baadhi yao wakidai kuwa sheria zilizopo zinakandamiza na kuwanyima kupata habari. Vikao hivyo vya bunge vitamalizika Aprili Mosi, mwaka huu.

Imelda Mtema
Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu amefunguka kwa mara ya kwanza na kusema kuwa hata yeye anampa pongezi mpenzi wake wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa jitihada alizozifanya mpaka kufikia hatua ya kumaliza nyumba yake iliyopo Madale jijini Dar.
Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Wema alisema kuwa hata kama hawako pamoja lakini kama kuna kitu cha kumsifia kwa jambo zuri alilofanya hana sababu ya kukaa kimya na akinyamaza atakuwa mnafiki.
“Nikikaa kimya bila ya kumpongeza Chibu nitakuwa mnafiki, amefanya jambo zuri la kuigwa hivyo binafsi nampongeza kwa hapo alipofikia,” alisema Wema ambaye katika hatua za mwanzo za ujenzi huo alishiriki.
Next PostNewer Posts Previous PostOlder Posts Home